Mhubiri Mlango 1 Ecclesiastes

Mhubiri 1:1 Ecclesiastes 1:1

Maneno ya Mhubiri mwana wa Daudi,mfalme katika Yerusalemu.

Mhubiri 1:2 Ecclesiastes 1:2

Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili.

Mhubiri 1:3 Ecclesiastes 1:3

Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua?

Mhubiri 1:4 Ecclesiastes 1:4

Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima.

Mhubiri 1:5 Ecclesiastes 1:5

Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake.

Mhubiri 1:6 Ecclesiastes 1:6

Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake.

Mhubiri 1:7 Ecclesiastes 1:7

Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena.

Mhubiri 1:8 Ecclesiastes 1:8

Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.

Mhubiri 1:9 Ecclesiastes 1:9

Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua.

Mhubiri 1:10 Ecclesiastes 1:10

Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi.

Mhubiri 1:11 Ecclesiastes 1:11

Hakuna kumbukumbu lo lote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lo lote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye.

Mhubiri 1:12 Ecclesiastes 1:12

Mimi, Mhubiri, nalikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu.

Mhubiri 1:13 Ecclesiastes 1:13

Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake.

Mhubiri 1:14 Ecclesiastes 1:14

Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo.

Mhubiri 1:15 Ecclesiastes 1:15

Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa, Wala yasiyokuwapo hayahesabiki.

Mhubiri 1:16 Ecclesiastes 1:16

Nikatafakari nikisema, Nimejipatia hekima nyingi kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; naam, moyo wangu umeona kwa wingi hekima na maarifa.

Mhubiri 1:17 Ecclesiastes 1:17

Nikatia moyo wangu ili kuijua hekima, na kujua wazimu na upumbavu; nikatambua ya kwamba hayo yote nayo ni kujilisha upepo.

Mhubiri 1:18 Ecclesiastes 1:18

Yaani, Katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni,Naye aongezaye maarifa huongeza masikitiko.